KAMBI YA HALIMA MDEE YAMEGUKA | +255 kwanza
Breaking News
Loading...

Thursday, 23 July 2015

KAMBI YA HALIMA MDEE YAMEGUKA


KAMBI ya aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), imeanza kusambaratika baada ya wafuasi wake kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo.Wafuasi wake hao wakiongozwa na diwani aliyemaliza muda wake katikaKata ya Kunduchi, Janeth Rithe, wamejiunga jana ACT-Wazalendo nakukabidhiwa kadi na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa.


Wengine waliopewa kadi za ACT ni Mary Mongi aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bawacha, Jimbo la Kawe, James Wambura (Katibu wa mbunge Kawe) na Manase Busa aliyefanikisha kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Mdee anaingia bungeni katika uchaguzi wa 2010.Wamo pia Katibu Bawacha Tawi la Wazo, Modesta Kalukula na Sizya Issa, Yamoyo Salehe, Sheilah Khamis, Tabia Mohamed, Ashura Salehe, Sophia Makoba na Fatuma Mikidadi.


Mbali na hao, chama hicho pia kimepokea wanachama wengine 198 kutoka CCM, Chadema na NCCR-Mageuzi waliojiunga kutoka jimbo hilo.Akizungumza baada ya kuwapokea, Msafiri alisema wanachama hao wameungana ili kuendeleza uzalendo kwa Taifa, hivyo chama hicho kinawakaribisha na wengine.
Kabwe Zuberi Zitto (born 24 September 1976), popularly known as Zitto Kabwe, is a Tanzanian politician.He was a member of the opposition party, Chadema, from 1992 until his expulsion in March 2015. He served as a Member of Parliament for the Kigoma North constituency from 2005 to 2015.On 20 March 2015, he officially joined the Alliance for Change and Transparency.

google+

linkedin

Malunde1 Blog
  • Karibu katika Mtandao wetu unatoa Habari Moto moto kutoka Ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga.Kama una Tangazo,Picha,Habari,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0688405951. Soma Zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    IDADI YA WASOMAJI WETU

    TAFUTA HABARI HAPA